Licha ya kuongezwa kwa muda wa wiki tatu wa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Lebanon yaliyotangazwa na Donald Trump siku ya Alhamisi, Aprili 23, mvutano unaendelea kati ya Israel na Hezbollah, ambayo haionyeshi dalili yoyote ya kulegeza msimamo wake: Kundi hili la wanamgambo wa Kishia linalounga mkono Iran linaendelea kupinga mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Beirut na Tel Aviv na kukataa kuweka chini silaha zake.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wakati Rais wa Marekani Donald Trump akitangaza siku ya Alhamisi, Aprili 23, kuongezwa kwa muda wa wiki tatu kwa makubaliano ya usitishaji mapigano kati ya Israel na Lebanon na kusema anatarajia mkutano kati ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Rais wa Lebanon Joseph Aoun “katika wiki zijazo,” Hussein Hajj Hassan, mbunge wa Hezbollah nchini Lebanon, amezungumzia kuhusu tangazo hili.

Alipoulizwa kwa mara ya kwanza kuhusu makubaliano yenyewe ya kusitisha mapigano, aliweka masharti kutokana na mwenendo wa Israel: “Ikiwa Israel itaheshimu kikamilifu makubaliano ya usitishaji mapigano, sisi pia tutaheshimu. Ikiwa Israel haitaheshimu na kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano, upinzani ni haki ya watu iwapo kutatokea uvamizi na mashambulizi,” alisema, huku pia akikataa kutaja ni wapiganaji wangapi kutoka kundi la kijeshi la Hezbollah wameuawa katika wiki za hivi karibuni.

Hezbolaah yapinga kupokonywa silaha na mazungumzo ya moja kwa moja 

Kuhusu kupokonywa silaha kwa kundi hili, ambapo serikali ya Lebanon ilijitolea mwaka jana, Hussein Hajj Hassan anaona ombi hili kuwa la mapema na anapinga hoja ya mamlaka: “Ni ajabu kweli kwamba taifa, serikali, linaomba kupokonywa silaha kwa upinzani kabla ya wanajeshi wa Israel kuondoka, kabla ya kukomesha uvamizi wa Israel, kabla ya kutimiza uhuru wa taifa hilo juu ya eneo lake,” ameongeza, akibaini kwamba mzozo na taifa la Israel haujaisha.

Kuhusu mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Lebanon na Israel, mbunge huyo ameibua wasiwasi kuhusu mvutano ambao mazungumzo kama hayo yanaweza kusababisha nchini Lebanon: “Sera ya Marekani iko wazi: inalenga kuunda na kukuza mvutano, ambao sio sera ya Hezbollah,” amesema.

Nchini Lebanon, wapinzani wa kisiasa wa kundi hili la Kishia linalounga mkono Iran wanaishutumu kwa kuiingiza nchi hiyo vitani kwa kuishambulia Israel mnamo Machi 2.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *