Wakuu wa Mihimili Mitatu ya Iran wamejibu madai ya uongo ya Rais Donald Trump Marekani kwamba kuna mgawanyiko ndani ya nchi na kusema: Hatuna watu wenye msimamo mkali na wenye msimamo wa wastani; sote ni Wairani na wanamapinduzi.

Wakuu wa Mihimili Mitatu ya Dola yaani Rais wa nchi, Spika wa Bunge na wa Mkuu wa Idara ya Mahakama nchini Iran wameandika katika ujumbe uliosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba: Hakuna watu wenye msimamo mkali na wenye msimamo wa wastani katika Iran yetu; sote ni Wairani na wanamapinduzi.

Masoud Pezeshkian, Mohammad Baqer Qalibaf na Hujjatul Islam Walmuslimin Gholamhossein Mohseni Ejei, wameandika ujumbe huo kujibu madai ya uongo ya Trump na kusisitiza kwamba: kwa umoja madhubuti wa taifa na serikali, na kwa utiifu kamili kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, tutamfanya mhalifu ajutie (makosa yake).

Katika ujumbe huo, uliochapishwa kwenye mitandao ya kijamii, wakuu wa mihimili mitatu ya Iran wameongeza kwamba Mwenyezi Mungu Mmoja, kiongozi mmoja, taifa moja, na njia moja; nayo ni njia ya ushindi wa Iran ambayo ni ina thamani kuliko uhai wetu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *