Jeshi la Nigeria limetangaza kuwa limeuwa magaidi 25, akiwemo kamanda wao wa ngazi ya juu katika hujuma ya magaidi hayo iliyozimwa na jeshi dhidi ya jamii moja kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Magaidi hao wa kundi la ISWAP wenye mfungamano na la Boko Haram walipanga kufanya shambulio katika eneo la Kukareta katika Jimbo la Borno muda mfupi baada ya saa sita usiku wa kuamkia Alhamisi lakini walishindwa kutekeleza hujuma hiyo baada ya kufurushwa na jeshi.

Meja Jenerali Abdulsalam Abubakar mmoja wa makamanda wa jeshi laNigeria amewaambia waandishi wa habari kwamba askari wao waliwakabili waasi katika mapigano yaliyoendelea hadi alfajiri kwa wakati wa Nigeria siku ya Alhamisi.

Kamanda wa ngazi ya juu wa kundi la kigaidi la ISWAP kwa jina la Abu Umar Bundi Muznir ni miongoni mwa magaidi waliouawa na jeshi la Nigeria kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *