Umoja wa Falme za Kiarabu uliwapa mamluki wa Colombia kulisaidia kundi la wanamgambo wa Sudan, la Rapid Support Forces (RSF), kuwaua maelfu ya raia katika nchi hiyo ya kaskazini mashariki mwa Afrika.

Taarifa hii imetolewa na Televisheni ya BBC ikinukuu uchunguzi wa Kundi la Conflict Insights (CIG) ambalo limekusanya data kutokana na kufuatilia simu za mkononi za mamluki wa Colombia.

Mkurugenzi wa kundi hilo la CIG, Justin Lynch ameiambia televisheni ya BBC kwamba uchunguzi uliofanywa na taasisi hiyo ya uchunguzi wa usalama ni wa kwanza ambapo tunaweza kuthibitisha kwa uhakika kuhusika kwa UAE katika mzozo wa Sudan.

 “Tunatamka wazi kile ambacho serikali zinajua kwa muda mrefu kuhusu uhusiano wa moja kwa moja kati ya Abu Dhabi na RSF,” amesema Justin Lynchi, Mkurugenzi wa Kundi la Conflict Insights (CIG).

Wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) waliuteka mji wa el-Fasher Oktoba 26, mwakka jana huku ripoti zikisema kuwa walifanya mauaji ya maelfu ya raia ambao walishindwa kukimbia makazi yao baada ya kutekwa na waasi wa RSF.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *