
Waziri wa mMmbo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi, akizungumza kutoka Moscow, ameishutumu Marekani kwa kushindwa kwa mazungumzo nchini Pakistan.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Waziri wa Mambo ya Jje wa Iran Abbas Araghchi ameishutumu Marekani Jumatatu kwa kuhusika na kushindwa kwa mazungumzo ya amani nchini Pakistan, baada ya kufika Urusi ambapo anatarajia kukutana na Rais Vladimir Putin.
“Mbinu za Marekani zilimaanisha kwamba duru ya awali ya mazungumzo, licha ya maendeleo fulani, haikufikia malengo yake kutokana na madai mengi,” amesema, akinukuliwa na vyombo vya habari vya serikali ya Iran. Pia amesema kwamba “usalama wa kupita kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz ni suala kubwa la kimataifa,” huku Marekani na Iran zikiendelea na kizuizi chao cha njia hii ya kimkakati majini.
Karibu wiki tatu baada ya kufikiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano baada ya siku 40 za mapigano kati ya Iran na Israel, mshirika wa Marekani, Moscow inasalia kuwa moja ya washirika wakuu wa Jamhuri ya Kiislamu. Bw. Araghchi anatarajia kukutana na rais wa Urusi, kulingana na shirika la habari la TASS, likimnukuu msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov.