
Jumapili, Aprili 26, ilikuwa siku ya misukosuko nchini Mali, siku chache tu baada ya kuanzishwa kwa mashambulizi yaliyoratibiwa kati ya waasi wa Azawad Liberation Front (FLA) na wanajihadi. Ingawa Bamako imekiri kifo cha Waziri wa Ulinzi, mamluki wa Urusi waliomba na kupokea ruhusa kutoka kwa watawala wapya wa Kidal kuondoka katika eneo hilo. raia, kwa upande wao, wana wasiwasi kuhusu vurugu hizo na wanahofia ukosefu wa utulivu mkubwa zaidi kuliko hapo awali.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Katika mkoa wa Kati, “utulivu unarudi hatua kwa kusuasua, lakini hakuna mfanyabiashara aliyethubutu kufungua duka lake” siku ya Jumapili. Mkoa wa Kati bado una athari ya mashambulizi hayo, hasa yale yaliyosababisha kifo cha Waziri wa Ulinzi Sadio Camara: washambuliaji walitumia lori lililojaa vilipuzi, wakigonga nyumba ya waziri na nyumba za jirani, ikiwa ni pamoja na msikiti ulio karibu. Mbali na Jenerali Sadio Camara, watu wengine kadhaa waliuawa.
Hata hivyo katika mkoa wa Kati, shughuli za kiuchumi zinachelewa kuanza tena. Kwa mfanyabiashara mmoja katika soko kuu la jiji, anasema hali hiyo si ya kutia moyo, kwani masoko yanaendelea kufungwa na wafanyabiashara wanaendelea kuishi kwa hofu.
“Utawala wa kijeshi unapaswa kukiri kushindwa; mazungumzo ya kitaifa yanapaswa kuanza,” limetangaza vuguvugu la upinzani, linaloongozwa na Imam Mahmoud Dicko.
“Mali iko hatarini.” Katika taarifa iliyotolewa jana, vuguvugu la upinzani, ambalo liko uhamishoni la Imam Mahmoud Dicko, ilimeelezea wasiwasi wake kuhusu hali nchini Mali.
“Mkanganyiko uliopo haupaswi kuficha jambo muhimu: Mali imepitia tu hali nyingine inayoonyesha kushindwa kudhibiti hali ya usalama,” limetangaza vuguvugu la Imam Mahmoud Dicko, linalojumuisha wanasiasa wanaopinga utawala wa kijeshi, ambalo “linalaani mashambulizi yote dhidi ya raia, maeneo ya umma, miundombinu muhimu, na mali ya raia.” linadai kujiuzulu kwa utawala wa kijeshi na “kuanzishwa mara moja kwa utawala wa mpito, utakaooongozwa na kiraia .”
Ofisi ya rais wa Mali haitakikuzungumza kilichotokea
Rais wa Mpito aanasalia kimya. Kulingana na taarifa kutoka kwa mwandishi wetu wa kikanda, Serge Daniel, Jenerali Assimi Goïta alikuwepo Kati, eneo lililokumbwa na mapigano mengi siku ya Jumamosi na Jumapili.
Aliondolewa haraka katika msafara wa kijeshi hadi Kambi ya Samanko, kituo cha mafunzo cha vikosi maalum anachotoka, tangu wakati huo inaripotiwa kwamba ameondoka kambini na, kulingana na wale walio karibu naye, yuko salama salimi. Hata hivyo, hakuna taarifa iliyotolewa kuhusu hali yake ya sasa.