Mwakilishi wa cha cha Democratic wa California katika Kongresi ya Marekani, Sara Jacobs, amemkosoa vikali Waziri wa Vita wa nchi hiyo, Pete Hegseth kwa kutangaza ushindi dhidi ya Iran, akitaja madai hayo kuwa ni udanganyifu.

Jacobs ambaye alikuwa akizungumza kwenye kikao cha maswali na majibu cha Kongresi ya Marekani kilichomwita Hegseth kujadili vita dhidi ya Iran, amemwambia Waziri huyo wa Vita kwamba: “Ikiwa unadhani hali ya sasa nchini Iran ni ishara ya ushindi, labda tunapaswa kuhoji afya yako ya akili.”

Seneta Chris Van Halen pia amekosoa sera za Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Iran na kusisitiza kwamba uamuzi wake wa kufuta mapatano ya nyuklia (JCPOA) umefungua njia ya vita dhidi ya Iran. Van Halen ameonya kwamba kuendelea na sera hii kumeiweka Marekani kwenye njia ya vita visivyoisha na Iran.

Wakati huo huo Steven Starr, profesa katika Chuo Kikuu cha Missouri amesema: “Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa pigo kubwa na la kulemaza kwa uwepo wa kijeshi wa Marekani katika eneo la Magharibi mwa Asia.”

Profesa Steven Starr amesema: “Marekani imefukuzwa kivitendo katika Ghuba ya Uajemi, karibu kambi zake zote za kijeshi zimeharibiwa au kuatilika na kambi kuu 13 hadi 19 zimeachwa au kuharibiwa kabisa.” Ameongeza kuwa: “Makao makuu ya Kamandi Kuu ya Kikosi cha Tano nchini Bahrain yalipigwa vibaya kiasi kwamba wanajeshi chini ya 100 wamesalia huko, na kambi zote za kijeshi za Marekani nchini Syria zimetelekezwa.”

Wakati huo huo, Seneta wa Vermont Bernie Sanders, ametoa takwimu za gharama kubwa za vita vya Marekani dhidi ya Iran na kuifichua kwamba vita hivyo vimeigharimu Washington dola bilioni elfu moja (trilioni moja), ambazo amesema zingeweza kutumika kwa ajili ya ustawi wa watu wa Marekani.

Sanders kisha amesema kwa kejeli kuhusu hali ya kiuchumi ya watu wa Marekani kwamba: Daima kuna fedha kwa ajili ya vita, lakini hakuna fedha za kutosha kwa ajili ya makazi, elimu au mahitaji ya tabaka la wafanyakazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *