Uchunguzi mpya wa CNN: Kambi nyingi za Marekani Asia Magharibi ziliharibiwa katika mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran

Kwa mujibu wa uchunguzi huo ambao matokeo yake yaliripotiwa na CNN siku ya Ijumaa, takriban maeneo 16 ya kijeshi ya Marekani katika nchi nane za magharibi mwa Asia yalishambuliwa kwa makombora na ndege za zisizo na rubani za Iran.

Katika mashambulizi kadhaa, uharibifu ulikuwa mkubwa sana na kuharibu kabisa zana za kijeshi za Marekani na kwamba maeneo mengi yaliyoharibiwa yalikuwa kambi za Marekani.

CNN imeweka wazi matokeo ya uchunguzi wake haya baada ya kuchunguza makumi ya picha za satelaiti na kufanya mahojiano na vyanzo vya habari nchini Marekani na katika mataifa ya Kiarabu ya Ghuba ya Uajemi.

Chanzo kingine cha habari nchini Marekani kimeeleza kuwa “hakijawahi kushuhudia uharibifu kama huu (uliosababishwa na mashambulizi ya Iran) huko nyuma.”

Wakati huo huo, picha za satelaiti zilizokaguliwa na CNN zimeonyesha kuwa mashambulizi ya Iran yalilenga mali za kijeshi za thamani ya juu, ikiwa ni pamoja na mifumo ya rada, miundombinu ya mawasiliano na ndege za aina mbalimbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *