
Watu watatu waliopatikana na hatia ya kuhusika katika ghasia na machafuko makubwa, mashambulizi dhidi ya askari usalama, na kuwa na uhusiano na Shirika la Ujasusi la Israel (Mossad) wamenyongwa katika mkoa wa Khorasan Razavi, kaskazini mashariki mwa Iran.
Wahalifu hao, Mehdi Rasouli, Mohammadreza Miri na Ebrahim Dowlatabadinejad, walinyongwa katika mji mtakatifu wa Mashhad Jumatatu asubuhi baada ya taratibu za kimahakama kukamilika na hukumu za mwisho kupitishwa na Mahakama ya Juu ya Iran.
Watu hao waliopatikana na hatia wamenyongwa Jumatatu asubuhi katika mji mtakatifu wa Mashhad baada ya Mahakama ya Juu ya Iran kupitisha hukumu za mwisho.
Kwa mujibu wa nyaraka za kesi hiyo, Rasouli na Miri waliokuwa wakishirikiana na Mossad, walishiriki kikamilifu katika ghasia na vitendo vya uharibifu na walihusika moja kwa moja katika mauaji ya afisa wa polisi Hamidreza Yousefinejad.
Naye Dowlatabadinejad alikuwa miongoni mwa wachochezi wakuu wa vitendo vya ugaidi katika kitongoji cha Tabarsi katika mji wa Mashhad, ambavyo vilisababisha kuuawa askari usalama kadhaa.
Rasouli na Miri walipatikana na hatia ya kuwasiliana na maafisa husika wa adui ili kudhoofisha usalama wa taifa la Iran kwa kuharibu mali za umma, kufanya hujuma, kuitisha mikusanyiko na mikutano haramu, kuwarushia polisi mabomu ya mkono na kutumia visu na silaha nyingine baridi, kuchochea ghasia na kuwashambulia askari polisi, kuharibu kituo cha basi na kuhusika moja kwa moja na mauaji ya polisi.