
Chumba cha uchunguzi cha Mahakama ya Rufaa ya Paris kimeamua Jumatano, Mei 6, 2026, kubatilisha kufutwa kwa mashtaka yaliyotolewa mwaka jana kwa mke wa rais wa zamani wa Rwanda, Agathe Habyarimana, aliyezaliwa Kanziga. Hapo awali kikao hicho kilipangwa kufanyika Aprili 8, lakini Mahakama ya Rufaa iliomba kuahirishwa kwa majadiliano bila kutoa maelezo zaidi.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mahakama ya Rufaa ya Paris imetoa uamuzi kuhusu hatua zinazofuata katika kesi ya mke wa rais wa zamani wa Rwanda, Agathe Habyarimana, ikibatilisha kufutwa kwa mashtaka yaliyotolewa mwaka jana na kuagiza uchunguzi uendelee. Mnamo mwezi Agosti mwaka uliyopita, mahakimu wawili wa Paris walibaini kuwa kulikuwa na “ushahidi wa kutosha” dhidi ya Agathe Habyarimana. Chumba cha uchunguzi cha Mahakama ya Rufaa kimeona uamuzi huu kuwa na makosa na kwa hivyo kimerudisha kesi hiyo kwa majaji wanaochunguza.
Mjane wa rais wa zamani kutoka kabila la Wahutu Juvénal Habyarimana amekuwa chini ya uchunguzi nchini Ufaransa tangu mwaka 2008 kwa “kushiriki katika mauaji ya kimbari” na “uhalifu dhidi ya ubinadamu.”
Kushiriki katika “Akazu”
Sababu zilizoandikwa za uamuzi huu zitatumwa kwa mawakili baadaye. Lakini Patrick Baudoin, wakili wa Shirikisho la Kimataifa la Haki za Binadamu (FIDH), amekaribisha uamuzi huo akisema ni kama “ushindi wa ukweli, wa haki, na dhidi ya kutokujali, hali ambayo ilikuwa imetawala kwa miaka mingi.”
Kulingana na vyama vya kiraia, Mke wa rais aliongoza “Akazu,” kundi al viongozi wa Kihutu wenye ushawishi mkubwa na wenye nguvu, linaloamua kinachotakixa kufanyika nchini. Inadaiwa alishiriki kikamilifu katika kupanga na kutekeleza mauaji dhidi ya Watutsi. “Vyama vyote vya kiraia na upande wa mashtaka vinabainisha kwamba kulikuwa na ushahidi wa kutosha kumfikisha mahakamani Agathe Havyaeimana,” amesema Emmanuel Daoud, wakili wa FIDH katika kesi hii.
“Kwa maoni yetu, alishiriki katika kuandaa orodha ya majina ya watu wa kabila la Wahutu wenye msimamo wa wastani na Watutsi ambao wangeuawa.” Mashahidi kadhaa wanamhusisha katika mikutano ya kupanga vitendo vya mauaji ya kimbari ndani ya Akazu. Kwa hivyo, kutokana na masharti ya amri iliyoandikwa na mahakimu wawili wa uchunguzi, sisi, kama vyama vingine vya kiraia, tuliona ni muhimu kukata rufaa,” ameongeza.
Vyama vya kiraia na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Kitaifa wa Kupambana na Ugaidi (PNAT) vinaamini, haswa, kwamba majaji walipuuza baadhi ya shuhuda muhimu na vipengele vya kihistoria katika kesi hii. Wakati huu, vyama vya kiraia vinatumai kuanza tena kwa kesi, ikiwa ni pamoja na kusikilizwa upya kwa kesi ya mke huyo wa rais zamani, ambaye kwa sasa ni shahidi msaidizi tu, na uchunguzi ufanyike nchini Rwanda.
Si “mhalifu” bali “mwathirika,” kulingana na mahakama
Katika uamuzi wao wa mwezi Agosti 2025, Agathe Habyarimana aliwasilishwa “si kama mhalifu wa mauaji ya kimbari, bali kama mwathirika” wa shambulio baya dhidi ya ndege ya mumewe Juvénal Habyarimana mnamo Aprili 6, 1994, ambalo, ikumbukwe, lilisababisha mauaji ya kimbari yaliyosababisha zaidi ya waathiriwa 800,000—Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani—nchini Rwanda.
Kwa sasa, Agathe Habyarimana bado ana hadhi nzuri zaidi ya kuwa shahidi msaidizi na hajashtakiwa rasmi, anabainisha wakili wake Philippe Meilhac, ambaye amekatishwa tamaa na utaratibu ambao “umekwama” kwa miaka ishirini, huku mteja wake sasa akiwa na umri wa zaidi ya miaka 83.