Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir amemuachisha kazi waziri wa fedha na mkuu wa majeshi ikiwa ni muendelezo wa mabadiliko ambayo amekuwa akiyafanya katika utawala wake.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Waziri Salvatore Garang Mabiordit ameachishwa kazi kama waziri wa fedha miezi mitatu baada ya kuteuliwa katika wadhifa huo, huku Kuol Daniel Avule akiteuliwa kujaza nafasi hiyo, mabadiliko yanayofanyika kipindi hiki nchi hiyo ikiripotiwa kupitia hali ngumu kiuchumi.

Rais Kiir pia amemuachisha kazi mkuu wa majeshi nchini humo, Jenerali Paul Nang Majok, na kumteua Jenerali Santino Deng Wol, aliyewahi kuhudumu katika wadhifa huo kuanzia mwaka 2021 hadi mwaka 2024, kuwa mrithi wake, hatua ambayo pia inaendelea kuibua hali ya sintofahamu katika uongozi wa jeshi nchini humo kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Kiongozi huyo mpya wa jeshi yupo chini ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa tangu mwaka 2015, kutokana na kile Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linasema kuwa amekuwa kikwazo kwa maridhiano nchini humo.

Mabadiliko haya yanaendelea kufanyika wakati serikali ya Sudan Kusini ikijiandaa kwa uchaguzi ambao umepangwa kufanyika mwezi Disemba mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *