Mvutano kati ya Iran na Marekani umeongezeka tena baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kukataa masharti yaliyowekwa na Iran kabla ya kuanza mazungumzo kuhusu madini yake ya urani yaliyorutubishwa.
Iran inataka mali zake zilizozuiliwa nje ziachiwe, vikwazo katika Mlango wa Bahari wa Hormuz viondolewe, na vita vinavyoendelea katika Mashariki ya Kati vikomeshwe kabla ya mazungumzo yoyote kuanza.
Kwa upande mwingine, Marekani na Israel zinasisitiza kuwa madini ya urani yaliyorutubishwa yaondolewe Iran ili kuzuia taifa hilo kupata uwezo wa kutengeneza silaha za nyuklia siku zijazo.
Wakati mkwamo huo ukiendelea kuongeza hofu ya kurejea kwa mapigano, Trump anatarajiwa kutumia ziara yake nchini China kumshawishi Rais Xi Jinping kusaidia kuishinikiza Iran kufikia makubaliano. China imethibitisha ziara hiyo ya Rais Trump inayotarajiwa kufanyika kati ya tarehe 13 hadi 15 mwezi huu.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)