Viongozi wa Afrika, wawekezaji na wadau wa biashara wanaoshiriki mkutano wa Africa Forward kati ya Ufaransa na Afrika, wametoa wito wa kuondolewa vikwazo vya kibiashara na uwekezaji ambavyo vimeendelea kupunguza kasi ya ukuaji wa uchumi wa bara hilo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwenya majadiliano hayo, maswala ibuka  yanayosibu Afrika ni gharama ya juu unaochangiwa na usalama mdogo , ushuru mkubwa na mazingira yayoyosua sua na kuwafukuza wawekezaji.

Paul Waweru ni afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya Ecomobilus ya Kwanza kuzalisha  mkokoteni ya umeme

“Huu mkokoteni unaweza kwenda pande zote mbili,yule ambaye ni dereva anaweza kuzungusha kiti kama kile cha kinyozi. ” Alieleza Paul Waweru.

Nafasi ya wanawake na wasichana haswa kwenye mataifa yenye migogoro imepata pia nafasi. Denis Mambo anatokea DRC.

“Sababu nimehudhuria Africa Forward Summit kuonesha biashara yangu mabapo natengeneza viatu kwa kutumia Crotchet nikitumia tairi zilizotupwa kutengeneza.” Alisumilia Densi Mambo.

Vile vile mchango wa sanaa na michezo. Cynthia Nandwa anahudumu katika shirika Boxgirls la wasichana wanaojihusisha kwenye ndondi jijini Nairobi.

“Michezo yao tunaweka wakati shule zimefungwa kwa hiyo hatusumbui masomo, lakini pia tunahamasha pia wajiunge na mchezo wa ndondi kama njia ya kujilinda na pia.” Alisistiza Cynthia Nandwa.

Mikataba  kadhaa ya kibiashara hadi shilingi bilioni moja imeshatangazwa na maazimio ya kongano hili yanayazamiwa pia kuwasilishwa kwenye kongamano la G7 linalofanyika Ufaransa mwezi Juni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *