Wito wa kuheshimiana ulitawala Mkutano wa Afrika Forwad kati ya Ufaransa na Kenya, huku Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akitangaza uwekezaji mpya na kusema uhuru utakuwa muhimu katika ushirikiano ambao Ufaransa inatarajia kujenga na Afrika.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Uwekezaji wenye thamani ya euro bilioni 23 (dola bilioni 27) utafadhili sekta mbalimbali barani Afrika ikiwa ni pamoja na nishati, akili unde na kilimo, Rais Macron akiongeza kuwa kuwa euro bilioni 14 (dola bilioni 16.4) zitatoka kwa makampuni ya Ufaransa na euro bilioni 9 (dola bilioni 10.5) zitatoka kwa mashirika ya Afrika.
Macron amesema mkutano huu unaashiria mabadiliko ya kifedha katika uhusiano kati ya Ulaya na nchi za Afrika, ikiwa ni pamoja na zile ambazo hapo awali zilikuwa makoloni yake.
Rais William Ruto wa Kenya, ambaye ameandaa mkutano huu pamoja na Ufaransa, alitaja neno uhuru kwa zaidi ya mara nane katika hotuba yake ya siku ya mwisho ya mkutano huo.
Rais Ruto amesema siku za Afrika kuitegemea Ulaya zimekwisha akitaka uhusiano wa heshima kwa pande zote.
Mkutano huu umetamatika jioni hii ambapo wakuu wan chi 30 waloshiriki kongamano hili walitia Saini, azimio ambalo limekuja wakatik huu Ufaransa ikiwa haina uhusiano mzuri na mataofa matatu ya ukanda wa Afrika Magharibi.