
Chuo Kikuu cha Kimataifa cha al-Mustafa kimetangaza kuwa ushiriki, uwezeshaji na ushirikiano wa UAE katika vita vya hivi karibuni vya Marekani na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Iran ni sawa na “kusaidia kambi ya ukafiri dhidi ya ndugu Waislamu” na hivyo, “kimsingi ni haramu.”
Chuo Kikuu cha Kimataifa cha al-Mustafa, seminari ya kimataifa ya wanafunzi wa kigeni yenye makao yake makuu katika mji wa Qum, kimetoa tamko hilo kujibu msimamo dhidi ya Iran uliopitishwa na Chuo Kikuu cha al-Azhar chenye makao yake makuu nchini Misri.
Wakati wa vita vya uchokozi vya muungano wa kijeshi wa Marekani na Israel, vilivyoanza Februari 28, Iran ilijibu kwa mashambulizi makubwa ya makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya maslahi ya Marekani na Israel katika eneo la Mgharibi mwa Asia, hasa yale yaliyoko katika nchi za Ghuba ya Uajemi, ikiwa ni pamoja na UAE.
Hata hivyo, Chuo Kikuu cha al-Azhar kilionekana kuikosoa Tehran na kulaani kile kilichokitaja kama “mashambulizi yasiyo na msingi” ya Iran dhidi ya UAE na nchi nyingine za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi, kikitaka kusitishwa mara moja mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran dhidi ya mali na maslahi ya Marekani katika nchi za Kiarabu ya Ghuba ya Uajemi.
Taarifa ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha al-Mustafa imeongeza kuwa “Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haijawahi kuanzisha vita yoyote, na hatua zake za kijeshi za hivi karibuni zilikuwa jibu halali na la kujilinda la kukabiliana na mashambulizi yaliyofanywa dhidi ya usalama na ardhi ya Iran kwa kutumia vibaya ardhi na anga za baadhi ya nchi jirani, ikiwa ni pamoja na UAE.”
Pia kimesisitiza sera ya Iran na kushikamana na busara, diplomasia na kanuni ya ujirani mwema, kikitoa wito kwa Chuo Kikuu cha al-Azhar kuhukumu yanayojiri kwa msingi wa Qur’ani Tukufu na Sunah badala ya kuathiriwa na “anga ya vyombo vya habari na wanasiasa wanaoegemea upande wa Magharibi.”
Taarifa ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha al-Mustafa pia imesisitiza udharura wa kuzingatia maadili ya Kiislamu katika vita.
Taarifa hiyo imesema: “Katika operesheni zake za kulipiza kisasi, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran – tofauti na mwenendo wa kihalifu wa utawala wa Israel na washirika wake – haijawalenga raia wa kawaida na wasio na hatia au miundombinu muhimu ya raia, na operesheni hizo zililenga kambi za kijeshi za Marekani katika eneo la Maghariibi mwa Asia.”
Al-Mustafa International University Chuo imetoa wito kwa nchi zote za Kiislamu kuungana dhidi ya adui Mmarekani na Uzayuni, ikiwahimiza wasomi kote katika ulimwengu wa Kiislamu kuzuia utekelezaji wa njama za kuzusha migawanyiko za madola ya kibeberu.