Donald Trump aonya kuwa “muda unakwisha” kwa Iran huku maendeleo ya kutafuta amani yakikwamaDonald Trump aonya kuwa “muda unakwisha” kwa Iran huku maendeleo ya kutafuta amani yakikwama

Trump

Chanzo cha picha, Reuters

Rais wa Marekani Donald
Trump ameionya Iran kwamba “muda unakwenda” huku mazungumzo ya kumaliza vita
yakikwama.

“Ni bora waanze
kuchukua hatua haraka, la sivyo hakutakuwa na chochote kitakachosalia kwao,”
aliandika kwenye jukwaa lake la Truth Social. “MUDA NI WA MUHIMU!”

Ujumbe huo ulitolewa
wakati rais huyo alipotarajiwa kuzungumza na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin
Netanyahu siku ya Jumapili.

Vyombo vya habari vya
Iran viliripoti kuwa Marekani imeshindwa kufikia makubaliano ya maana katika
majibu yake kuhusu mapendekezo ya hivi karibuni ya Tehran ya kumaliza mzozo
huo.

Ukosefu wa maridhiano
kutoka Washington utasababisha “kukwama kwa mazungumzo,” shirika la habari la
nusu rasmi la Mehr liliripoti.

Rais huyo alionya
mapema wiki hii kwamba makubaliano ya kusitisha mapigano yalikuwa kwenye “hatua
mbaya sana ya kuendelea kuwepo” baada ya kukataa matakwa ya Tehran, akiyataja
kuwa “hayakubaliki kabisa.”

Esmail Baghaei,
msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran, alisisitiza kuwa mapendekezo hayo
yalikuwa “ya kuwajibika” na “ya ukarimu.”

Kwa mujibu wa shirika
la habari la nusu rasmi la Tasnim nchini Iran, mapendekezo hayo yalijumuisha
kusitishwa mara moja kwa vita katika maeneo yote, ikimaanisha mashambulizi
yanayoendelea ya Israel dhidi ya kundi la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran
nchini Lebanon, kusimamishwa kwa mzingiro wa kijeshi wa majini wa Marekani
kwenye bandari za Iran, pamoja na dhamana kwamba hakutakuwa na mashambulizi
mengine dhidi ya Iran.

Pia yalidaiwa
kujumuisha ombi la fidia kwa uharibifu uliosababishwa na vita na kusisitiza
mamlaka ya Iran kwa Mlango Bahari wa Hormuz.

Shirika la habari la
Fars nchini Iran lilisema Jumapili kuwa Washington iliweka masharti matano
kujibu pendekezo la Tehran.

Masharti hayo
yanadaiwa kujumuisha kuitaka Iran kubakiza kituo kimoja tu cha nyuklia
kikiendelea kufanya kazi na kuhamisha akiba yake ya urani iliyorutubishwa kwa
kiwango cha juu kwenda Marekani.

Unaweza kusoma;

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *