Chanzo cha picha, Reuters
Umati
wenye hasira ulichoma moto sehemu ya hospitali inayowashughulikia wagonjwa wa
Ebola mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya familia na marafiki wa
kijana aliyefariki katika hospitali hiyo kuchukua
mwili wake kwa nguvu kwa ajili ya mazishi.
“Walianza
kurusha mawe. Hata walichoma mahema yaliyokuwa
yakitumika kama wodi za kuwahifadhi wagonjwa waliotengwa,” mwanasiasa wa eneo
hilo, Luc Malembe, aliiambia BBC kuhusu tukio lililoshuhudiwa katika Hospitali Kuu ya Rwampara.
Polisi
walilazimika kufyatua
risasi hewani kuwatawanya waandamanaji.
Mwili wa mtu aliyefariki kutokana na Ebola huwa na uwezo mkubwa wa
kueneza ugonjwa huo, hivyo
mamlaka hulazimika kuhakikisha mazishi yanafanyika kwa njia salama ili kuzuia
kuenea kwa virusi hivyo.
Wahudumu wa afya katika hospitali ya Rwampara, iliyoko karibu na
mji wa Bunia katika jimbo la Ituri, ambako karibu visa vyote vya Ebola vimeripotiwa, wapo chini ya ulinzi wa jeshi huku
polisi wakijaribu kurejesha utulivu eneo hilo.
Jean Claude Mukendi, anayesimamia
uratibu wa usalama dhidi ya ugonjwa
Ebola eneo la Ituri, amesema kuwa kijana huyo aliyefariki
alikuwa maarufu katika jamii hiyo na
watu waliokuwa wameghadhabishwa na kifo chake hawaelewi
hatari wa ugonjwa huo.
Pia unaweza kusoma:
