
Mahakama Kuu ya Ndjamena imefutilia mbali siku ya Alhamisi, Mei 21, rufaa iliyowasilishwa na kundi la mawakili wa kiongozi wa zamani wa serikali, na hivyo kumfanya ahukumiwe kifungo cha miaka 20 jela kwa kutangaza, mnamo mwaka 2023, ujumbe ambao unadaiwa ulisababisha, miaka miwili baadaye, mapigano ya umwagaji damu kati ya jamii huko Mandakao, kulingana na mahakama nchini Chad.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko N’Djamena, Nadia Ben Mahfoudh
Uamuzi huo ulitolewa yapata saa 10 jioni kwa saa za Chad: siku ya Alhamisi, Mei 21, Mahakama Kuu ya N’Djamena ilikataa rufaa iliyowasilishwa na timu ya wanasheria ya Waziri Mkuu wa zamani wa Chad Succès Masra, na hivyo kuthibitisha kifungo chake cha miaka 20 jela kwa “kusambaza jumbe za ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya wageni,” “njama za jinai,” na “kushiriki katika mauaji.”
Kwa tukio hilo, polisi na wanajeshi wengi walitumwa kuzunguka jengo hilo, na kuzuia ufikiaji wa watu au wafuasi wa kiongozi huyo wa azamani wa serikali katika mahakama. Waandishi wa habari, haswa, waliamriwa kuondoka katika eneo hilo.
Hukumu hiyo ilitolewa na Mahakama ya Jinai mwezi Agosti mwaka uliyopita dhidi ya kiongozi wa zamani wa serikali na rais wa chama cha Les Transformateurs, pamoja na zaidi ya watu 70 walioshtakiwa kwa kushiriki katika mauaji ya Mandakao mnamo mwezi Mei 2025.
“Msemaji wa serikali alisema tangu mwanzo: kesi hii ni ya kisiasa tu!”
Succès Masra anashutumiwa, haswa, kwa kusambaza ujumbe mnamo mwaka 2023 ambao, kulingana na mahakama nchini Chad, ulisababisha mapigano ya umwagaji damu kati ya jamii yaliyotokea miaka miwili baadaye kusini mwa nchi. “Mahakama Kuu ilifutilia mbali rufaa yetu ingawa ilikuwa imetangaza kukubalika kwa misingi ya kiutaratibu. […] Tutaamua cha kufanya baadaye kwa wakati unaofaa,” alisema Francis Kadjilembembaye, mratibu wa timu ya wanasheria ya Succès Masra.
Claudia Hoinathy, naibu kiongozi anayesimamia Ushirikishwaji na Uongozi wa Wanawake katika chama cha Les Transformateurs, alisema kwa kushutumu uamuzi huo kama wa aibu. “Hatuwezi kukubaliana na hukumu kali kama hiyo dhidi ya mtu asiye na hatia. Msemaji wa serikali alisema tangu mwanzo: kesi hii ni ya kisiasa tu!” alisema, kabala ya kuongeza, “kwa hivyo tunatumai kwamba suluhisho la kisiasa litapatikana,” yaani, msamaha wa rais.”
Kisheria, njia pekee inayosalia kwa Succès Masra ni kupeleka kesi hiyo katika mahakama za kikanda au za kimataifa.
