Katika kipindi cha saa 24 zilizopita, ripoti zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii kudai kwamba Rais wa Iran Masoud Pezeshkian amejiuzulu kutokana na mvutano wa uongozi.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na ripoti hii, Pezeshkian amechukua hatua ya kujiuzulu baada ya kuibuka mvutano wa uongozi kati ya serikali yake na walinzi wa mapinduzi wa Iran.

Ripoti hizo zinasema Rais Pezeshkian amekuwa akitengwa katika masuala ya kutoa maamuzi kuhusu vita vya Iran.

Tehran imekanusha ripoti hizo ikizitaja kama za uongo na propaganda ya shirika moja la habari la kimataifa.

Ripoti hiyo ilichapishwa kwa mara ya kwanza na shirika la habari la Iran International, lenye makao yake jijini London ambalo wafanyikazi wake kwa sehemu kubwa ni raia wa Iran wanaoishi katika mataifa ya kigeni.

Soma piaRipoti iliochapishwa kudai kwamba Rais wa Iran amejiuzulu

Shirika hilo kwa sehemu kubwa limekuwa likionekana na serikali ya Iran kama chombo kinachotumiwa na wapinzani wake.

Katika ripoti yake, shirika hilo likinukuu vyanzo vya karibu na suala hilo, liliripoti kwamba Rais Pezeshkian aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa kiongozi wa kiroho wa Iran Ayatollah Mojtaba Jumapili ya wiki iliopita. 

Madai hayo pia yalichapishwa na vyombo vya habari vya Israel

Ripoti ya shirika hilo ilisema Rais wa Iran alikuwa amechoshwa na kile alichokitaja kama hatua ya jeshi la Iran kuingilia masuala ya serikali na kuhisi kwamba utawala wake ulikuwa umetengwa katika meza ya maamuzi muhimu.

Mashirika mengine ya habari ya kimataifa kama Fox News  ya nchini Marekani yalichapisha habari sawa na hiyo hali ambayo ilichangia habari hiyo kusambaa kwa kasi.

Soma piaShirika la habari la nchini Marekani Fox News nalo pia liliripoti habari hiyo

Mamlaka nchini Iran imesema ripoti hizo zinalenga kuleta mpasuko na ukosefu wa uthabiti nchini humo, ikiituhumu mashirika ya habari ya kimataifa kwa kuendeleza propaganda.

Licha ya kwamba Pezeshkian mwenyewe hajazungumzia madai ya kujiuzulu kwake, alinukuliwa na shirika la habari linalomilikiwa na serikali ya Iran Jumapili ya wikendi iliopita akisema ataendelea na majukumu yake hadi pumzi ya mwisho.

Soma piaMsemaji wa serikali ya IRAN akanusha ripoti za Rais wao kujiuzulu

Katika hatua nyengine, vyombo vya habari vya Japan vimeripoti kwamba amekuwa na mazungumzo ya njia ya simu na Waziri Mkuu wa Japan Jumatatu ya juma hili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *