Mtaalamu wa masuala ya Kiislamu kutoka Kenya katika mahojiano na Pars Today: Urithi wa Ayatullah Khamenei unaelekeza mwelekeo wa nchi za Kusini mwa Dunia katika harakati za kulinda heshima na uhuru wao.

Mtaalamu wa masuala ya Kiislamu kutoka Kenya anaamini kuwa urithi wa Ayatullah Khamenei katika nyanja za kujitegemea, kusimama kidete dhidi ya mashinikizo na utawala wa Kiislamu utaendelea kuwa dira inayounda mwelekeo wa nchi za Kusini mwa Dunia katika juhudi zao za kulinda heshima, utu na uhuru wao.

Dkt. Hasan Kinyua Ammari, mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka ishirini katika ufundishaji, uongozi wa maadili na mazungumzo ya tamaduni mbalimbali, pamoja na kuwa mtaalamu wa masuala ya Kiislamu, mshauri wa mazungumzo baina ya dini, mfasiri na mwandishi wa vitabu zaidi ya arobaini, amesema hayo katika mahojiano haya maalumu na Pars Today ambapo anatoa tathmini ya kina kuhusu maana ya kiroho na kisiasa ya urithi wa Ayatullah Khamenei na umuhimu wake wa kudumu kwa Waislamu duniani.

Shughuli za mazishi ya Ayatullah Sayyid Ali Khamenei zina maana ya kina ya kiroho, kidini na kihistoria. Kwa Waislamu wengi, hasa wale waliomtambua kuwa Imam mkubwa, kiongozi wa Waumini, mwanazuoni, faqihi na mlinzi wa utambulisho wa Kiislamu, mazishi yake si tukio la kumzika kiongozi wa kisiasa pekee. Ni wakati wa kutafakari kuhusu uongozi, kujitolea, hali ya kufa kwa mwanadamu na wajibu wa kila mtu mbele ya Mwenyezi Mungu.

Wawakilishi kutoka nchi zaidi ya 90, pamoja na viongozi wa kidini, wasomi, na watu mashuhuri kutoka kila pembe ya dunia, wanatarajiwa kushiriki katika shughuli za mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyed Ali Khamenei.

Mamlaka husika hapa nchini zimetangaza mapumziko ya umma ili kuwezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika hafla hizo za kihistoria, ambapo mkoa wa Tehran utakuwa na mapumziko kuanzia Julai 4 hadi 5, huku siku ya Julai 6 ikitangazwa kuwa siku ya kitaifa nchi nzima kwa ajili ya msafara mkuu wa mazishi jijini Tehran. Vilevile, mkoa wa Qom utakuwa na mapumziko siku ya Julai 7 wakati msafara wa mazishi utakapofika mkaoni humo. Halikadhalika mkoa wa Khorasan Razavi utaungana na ratiba hiyo siku ya Julai 9 ili kurahisisha utaratibu wa kutoa heshima za mwisho kwa Kiongozi Shahidi.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa mnamo Julai 8 mwili wa Kiongozi Shahidi utapelekwa nchini Iraq, ambapo mapokezi rasmi yatafanyika katika uwanja wa ndege wa Baghdad au Najaf, yakifuatiwa na maandamano na ibada maalum katika miji mitakatifu ya Najaf na Karbala.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *