
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amedai kwenye Fox News siku ya Jumapili, Julai 5, kwamba baadhi ya vijiji vya Wakristo kusini mwa Lebanon vimeomba Israel “viunganishwe.” Hakuvitaja vijiji hivyo. Kulingana na Benjamin Netanyahu, wakazi walikuwa wakitaka kujilinda dhidi ya Hezbollah inayounga mkono Iran.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Miongoni mwa vijiji vya Wakristo nchini Lebanon, baadhi vimeomba hata kuunganishwa na Israel, kwa sababu tunavilinda kutokana na vibaraka wa Hezbollah wanaotaka kuwaua. Na tunafanya vivyo hivyo na Wakristo kila mahali,” alisema kwenye kipindi cha “The Sunday Briefing.”
Meya wa kijiji cha Wakristo cha Rmeish, Hanna al-Amil, aliyenukuliwa na shirika la habari la serikali ya Lebanon ANI, alikanusha madai haya.
Kulingana naye, “maeneo 15 ya Wakristo yalitoa taarifa siku mbili zilizopita zikikanusha” madai hayo na kusisitiza “uaminifu wao kwa utambulisho wao wa kitaifa” na “kushikamana kwao na bendera yao ya Lebanon.” “Kufikiria wazo kama hili” haiwezekani kabisa,” alisema.
Lebanon iliingizwa katika vita vya Mashariki ya Kati mnamo Machi 2, wakati Hezbollah iliporusha makombora dhidi ya Israel kuiunga mkono Iran, ambayo ililengwa na mashambulizi ya Marekani na Israel.
Israel ililipiza kisasi kwa mashambulizi makali ya angani na mashambulizi ya ardhini kusini mwa Lebanon. Sasa inashikilia sehemu ya kusini mwa Lebanon karibu na mpaka.
Tangu mwanzo wa vita, baadhi ya vijiji vya Wakristo vimeathiriwa na mabomu ya Israel, na kulazimisha wakazi wake kukimbia.
Lakini vingi vilibaki na watu licha ya wito wa Israel wa kuhama. Jeshi la Israel lilikuwa limeonya vijiji kadhaa vyenye Wakristo wengi kutoruhusu wageni kuingia au kubaki, kwa usalama wao wenyewe.
Mkutano wa Trump na Netanyahu
Katika hotuba iliyotolewa katika sherehe siku ya Jumapili, Benjamin Netanyahu alibainisa kwamba jeshi litaendelea kuwapo “kwa muda mrefu iwezekanavyo ili kuwalinda wakazi wa kaskazini na raia wote wa Israel.”
Katika Fox News, pia alizungumzia kutokubaliana kwake na Donald Trump kuhusu mkataba wa makubaliano uliosainiwa Aprili 17 kati ya Washington na Tehran unaolenga suluhu ya kudumu ya mzozo wa kikanda, ambao unajumuisha Lebanon.