Msafara mkubwa usio na mfano wake wa mazishi adhimu na ya kihistoria ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu yamefanyika Jumatatu Tehran mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Msafara huo mkubwa wa makumi ya kilomita ulianza masaa kadhaa hata kabla ya kuanza kutekelezwa ratiba rasmi iliyotangazwa na serikali kwa ajili ya kuenzi na kumuaga rasmi Kiongozi Shahidi aliyeuwa kikatili na tawala za kigaidi za Marekani na Israel akiwa pamoja na maafisa wa ngazi za juu serikalini na jamaa wa karibu wa familia yake.
Mamilioni ya watu wamejitokeza kwa wingi kwa ajili ya kushiriki kwa hamasa katika ghughuli hiyo ya kitaifa, kwa namna ambayo uwepo wao kwa mara nyingine tena umedhihirisha, umoja mshikamano na utiifu usioyumba wa taifa la Iran kwa malengo matukufu ya Mapinduzi ya Kiislamu na kwa mashahidi waliojitolea mhanga maisha yao kwa ajili ya utu na uhuru wa mwanadamu.Kuanzia mapema alfajiri, bahari ya wafuasi wa dhati wa mujahid huyu aliyeuawa shahidi walimiminika katika mitaa ya Damavand, Barabara ya Imam Hossein, Enghelab, barabara ya Azadi, Uwanja mashuhuri wa Azadi, na kisha Barabara kuu ya Shahid Lashkari kwa ajili ya kumuaga kiongozi huyu mashuhuri ambaye alijitolea maisha yake kwa ajili ya kulinda Uislamu, Mapinduzi ya Kiislamu na Iran.
Jumatatu, mji wa Tehran umekuwa jukwaa la tukio kuu la kihistoria—ambapo mamilioni ya watu, wakiwa na sauti na kupiga hatua moja, huku wakitokwa na machozi na kupaza kaulimbiu zenye maana kubwa, wametoa buriani ya mwisho kwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyeuawa shahidi, na kupitia ushiriki wao wa kupigiwa mfano, wameufikishia ulimwengu ujumbe wa uthabiti, umoja, mshikamano na kuendelezwa njia ya mashahidi watukufu. Akizungumzia shakhsia na kujitolea kwa Shahid Ayatullah Khamenei katika njia ya kutetea na kulinda Uislamu na Mapinduzi ya Kiislamu, na vilevile ushiriki mkubwa wa wananchi katika mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Hossein Nouri-Hamedani, marja wa ngazi ya juu katika ulimwengu wa Uislamu amesisitiza hadhi ya juu na ya kipekee ya shahidi huyu, akisema: “Huenda leo hadhi hii bado haijawabainikia wengi kikamilifu lakini kwangu mimi nimemjua kiongozi huyu mwenye thamani kubwa ambaye tumempoteza; tangu miaka ya 1950, na maisha yake yote yalijaa vipengele muhimu, vyenye thamani, na vya kuzingatiwa.

“Akiashiria mwitikio mkubwa wa umma katika sherehe za kuaga na mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Iran, amesema:
“Katika siku chache zilizopita, dunia nzima imeshuhudia na kushangazwa na ukubwa wa idadi ya watu waliojitokeza, na, kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu, ushiriki huu utazidi kuenea katika siku zijazo.”Mwanazuoni huyu mashuhuri wa kidini katika ulimwengu wa Kiislamu imesisitiza zaidi kwa kusema: ‘Maadui wajue kwamba idadi hii kubwa ya watu inawakilisha sehemu ndogo tu ya wale waliopenda na kuunga mkono fikra zake. Shakhsia huyu ana wapenzi na wafuasi wengi kote ulimwenguni. Kila mtu lazima aelewe kwamba mgogoro upo kati yetu na mrengo wa kiburi duniani, ukiongozwa na Marekani na Wazayuni. Taifa hili halitawahi kukubali ukandamizaji, kwani utamaduni wetu wa kidini unatuzuia kujiunga na wakandamizaji na nguvu za kiburi.’Akilaani watekelezaji wa jinai hii, amesema: ‘Wote waliohusika watambue kwamba hawatakwepa adhabu ya jinai hii.’ Wakati huo huo, Mkuu wa Idara ya Mahakama nchini Iran ameapa kuwafuatilia na kuwaadhibu watawala wa Marekani na Israel kwa mauaji ya hayati Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei.
Gholam-Hossein Mohseni Ejei alitoa kauli hiyo siku ya Jumapili katika hafla iliyofanyika mjini Tehran kwa ajili ya kuzindua kitabu kinachohusu maisha na mitazamo ya Kiongozi mpya wa Iran, Ayatollah Seyyed Mojtaba Hosseini Khamenei; hafla iliyohudhuriwa na wageni kutoka nje ya nchi, wasomi, na wanaharakati.Amesema, “Kwa zaidi ya miezi minne, wananchi wetu, vijana kwa wazee, wamekuwa katika maombolezo ya kiongozi wao aliyeuawa shahidi na wamesimamisha bendera ya kudai kisasi cha damu.

Mkuu wa Vyombo vya Mahakama nchini amesema Marekani na Israel lazima zilipe gharama ya jinai zao dhidi ya taifa la Iran, akiongeza kuwa, mikataba yote ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na Mkataba wa Geneva, ina vifungu vilivyo wazi kuhusu jinai za kivita.”Tutawafuatilia bila kuchoka, kuwafikisha mahakamani na kuwaadhibu. Pia tutawalazimisha kufidia uharibifu waliofanya dhidi ya taifa la Iran,” amessisitiza.Mohseni Ejei ameongeza kuwa Iran itaendelea kuunga mkono Mhimili wa Muqawama kwa nguvu na azma yake yote, ikiwa ni pamoja na harakati yoyote iliyo dhidi ya Marekani na wakandamizaji wa Kizayuni.Mkuu wa Idara ya Mahakama pia amezitaka nchi jirani kutahadhari zaidi “nia mbaya na uovu wa maadui wa Uislamu,” akiongeza kuwa Iran inaziunga mkono nchi zote jirani mradi tu zizishirikiane na adui.