Idadi kubwa ya wapiga kura nchini Marekani wanaamini kuwa vita vya Donald Trump dhidi ya Iran havijazalisha tija inayostahili gharama zilizotumika. Kulingana na utafiti mpya wa gazeti la Financial Times, hali hiyo inaashiria jinsi mzozo huo unavyozidi kudhoofisha uungaji mkono kwa mtawala huyo kuelekea uchaguzi wa katikati wa muhula mwezi Novemba.

Utafiti huo wa kitaifa, uliofanywa wiki iliyopita na kampuni ya Focaldata, umebaini kuwa asilimia 58 ya wapiga kura waliosajiliwa walisema vita hivyo vilikuwa na gharama kubwa na havikuwafaidisha Wamarekani hata kidogo.

Aidha, asilimia 44 ya wapiga kura walieleza kuwa mzozo huo umeifanya Marekani kuwa katika nafasi duni zaidi dhidi ya Iran, ikilinganishwa na asilimia 31 pekee waliosema kuwa vita hivyo vimeimarisha nguvu za Washington.

Ikizingatiwa ukubwa wa gharama hizo, Ikulu imeliomba Bunge la Marekani kuidhinisha dola bilioni 67 za fedha za serikali ili kugharamia gharama za vita hadi sasa.

Utafiti wa FT pia umeonesha kuwa wapiga kura wana mashaka makubwa kuhusu makubaliano kati ya Washington na Tehran. Takriban asilimia 66, walisema makubaliano hayo hayataleta mabadiliko makubwa katika amani na utulivu wa eneo la Asia Magharibi, au huenda yakachochea ukosefu wa utulivu na kuongeza uwezekano wa migogoro zaidi.

Utafiti huo pia umeangazia jinsi vita hivyo, ambavyo vimesababisha kupanda kwa kasi ya bei ya mafuta na bidhaa nyingine za msingi mwaka huu, vinavyoendelea kushusha kiwango cha uungaji mkono kwa Trump.

Vita hivyo vya kikatili vilipelekea kuuawa shahidi Ayatullah Khamenei  Febrauri 28 sawa na 10 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika hujuma ya kigaidi ya Marekani  na Israel katika siku ya kwanza ya vita vya tawala hizo mbili dhidi ya Iran. Vita hivyo viliendelea kwa siku 40 ambapo Marekani ililazimika kuomba usitishaji vita kutokana na hujuma za kulipiza kisasi za Iran dhidi ya ngome za kijeshi na kiuchumi za Marekani na Israel katika eneo lote la Asia Magharibi.

3498116

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *