Leo imetimia miaka miwili tangu Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ilipotekeleza operesheni ya Kimbunga cha al-Aqswa na kutoa pigo kubwa na la kihistoria dhidi ya utawala haramu wa Israel.

Miaka miwili iliyopita katika siku kama ya leo ya tarehe 7 Oktoba, 2023, Operesheni yenye kuleta ghera na fakhari ya Kimbunga cha al-Aqsa iliendeshwa na wanamapambano wa Palestina wakiongozwa na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS na kutoa pigo kubwa mno la kihistoria kwa utawala wa Kizayuni wa Israel. Operesheni hiyo ya kishujaa na ya ya kushtukiza ilikuwa jibu la lazima la miongo kadhaa ya uvamizi wa kijeshi, kuzingirwa Ukanda wa Gaza na jinai za kibinadamu zinazofanywa na Israel dhidi ya Wapalestina. 

Operesheni ya kimbunga cha al-Aqsa ilifanyika katika eneo la mpaka kati ya Ghaza na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ambazo zimepachikwa jina bandia la Israel. Operesheni hiyo ilianza wakati wa alfajiri. Vikosi vya Hamas kwanza walipiga maeneo ya Wazayuni kwa kutumia maroketi na walirusha makombora 5,000. Baada ya hapo, walivuka ukuta uliojengwa na jeshi la Israel na kuingia kwenye maeneo ya walowezi wa Kizayuni. Taarifa zinasema kuwa, zaidi ya wanajeshi 1,400 wa Israel waliangamizwa na 3,500 wengine walijeruhiwa kwenye operesheni hiyo ya kishujaa.

Wanamapambano wa Hamas waliongoza operesheni kwa ufanisi wa hali ya juu kiasi kwamba hata walifanikiwa kukamata kundi la wanajeshi wa Kizayuni na kuwahamishia Ghaza kama ngawira. Operesheni hiyo ilikuwa ni pigo kubwa mno kwa Israel kwa namna ambayo haijawahi kutokea katika historia yake yote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *