Mgombea ubunge wa Jimbo la Maswa Mashariki kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Abel Mpina amezindua rasmi kampeni zake jimboni humo huku akiahidi ajira, barabara, maji safi na huduma bora za afya.

Uzinduzi wa kampeni hizo umefanywa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano wa chama hicho, Shangwe Ayo ambaye amewaeleza wananchi kuwa sera ya ACT-Wazalendo ni kumaliza tatizo la maji nchini ndani ya miaka mitano, ambapo kiasi cha shilingi trilioni 10 kitatengwa kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji nchini.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *