
Amesema kuwa mazungumzo yaliyopangwa kufanyika mchana yatashirikisha viongozi wa kiroho, wanafunzi, wawakilishi wa vijana, na makundi mengine.Jumatatu, Rajoelina alimteua Jenerali wa Jeshi Ruphin Fortunat Zafisambo kuwa Waziri Mkuu mpya, wiki moja baada ya kuwafuta kazi mawaziri wake wote katika hatua ya kushughulikia malalamiko yaliyochochea maandamano ya Septemba 25. Hata hivyo, mabadiliko hayo hayajawatuliza waandamanaji ambao awali walijitokeza mitaani kulalamikia uhaba wa maji na umeme katika taifa hilo maskini la Afrika, lakini sasa wanataka Rais Rajoelina ajiuzulu.