Rais wa Madagascar Andry Rajoelina amemteua Ruphin Fortunat Zafisambo, jenerali wa jeshi, kuwa waziri mkuu mpya wa nchi siku ya jumatatu, wiki moja baada ya kuvunja baraza la mawaziri.

“Kwa hekima kabisa, nimeamua kumteua Ruphin Fortunat Dimbisoa Zafisambo, Jenerali, kuwa Waziri Mkuu wa serikali,” kiongozi wa nchi amesema.

Hili linatokea wakati maandamano yakiingia wiki yake ya tatu siku ya Jumatatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *