
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, operesheni ya Kimbunga cha al-Aqswa iliyotokelezwa na wanamuqawama wa Palestina dhidi ya Israel iliipeleka dunia upande wa kuufuta “Umarekani” na kutetea wanaodhulumiwa.
Muhammad Baqir Qalibaf amesema hayo leo kwa mnasaba wa kutimia miaka miwili ya Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqswa na kubainisha kwamba, operesheni hiyo ilikuwa pigo la kistratijia kwa utawala wa Kizayuni na mahesabu ya ubeberu wa kimataifa, jambo ambalo liliifanya Israel kuzama katika kinamasi cha kushindwa.
Spika wa Bunge la Iran ameeleza kuuwa, kambi ya muqawama wa Palestina, Lebanon, Yemen na kujihami wananchi wa Iran wakiwa wameshikamana subira na ustahimilivu umeifikisha hali ya mambo katika eneo hadi kufikia kiwango ambapo Israel imekuwa utawala unaochukiwa zaidi duniani. Wazayuni katika sehemu nyingi za dunia wamepoteza amani kwa kuhofia makabiliano ya umma.
Spika Qalibaf amesema, hii leo mipaka ya kijiografia ya muqawama inaenea sio tu Gaza, Sanaa, na Beirut, lakini pia hadi Sydney, Berlin, Barcelona, Madrid, London, Amsterdam, Toronto, na miji na vyuo vikuu vya Marekani. Kampeni za kuususia utawala wa Kizayuni zimeenea duniani kote, na msafara wa kimataifa wa Sumud ni ishara ya kuenea muqawama duniani kote.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa: “Kimbunga cha al-Aqswa si tu kwamba ilivunja nguvuu bandia ya Israel, bali pia ilipeleka walimwengu kuelekea upande wa kuufuta “Umarekani” na kutetea wanaodhulumiwa kushindwa kikamilifu mradi wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.