Makamanda wa majeshi ya majini ya Iran, Russia, Kazakhstan na Azerbaijan wametia saini mkataba wa ushirikiano wa kimkakati unaolenga kuimarisha usalama katika maji ya pamoja.

Mkataba huo umesainiwa leo asubuhi katika mkutano wa mataifa manne ya eneo la Kaspi yenye ukanda wa pwani uliofanyika katika mji wa Saint Petersburg nchini Russia. 

Shahram Irani Kamanda wa jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameiwakilisha Tehran katika mkutano huo na kusaini hati yamakubaliano hayo kwa niaba ya Iran. 

Makubaliano hayo yanalenga kuimarisha ushirikiano wa kina kati ya nchi za eneo la Kaspi zenye ukanda wa pwani hasa katika kuhakikisha usalama unaimarishwa siku zote katika maji ya pamoja. 

Kwa mujibu wa masharti ya hati hiyo ya ushirikiano, nchi yoyote ajinani au dola lolote katika eneo halitaruhusiwa kuingilia masyala ya ndani ya Bahari ya Kaspi. 

Makamanda wa Majeshi ya Majini ya Iran, Russia, Kazakhstan na Azerbaijan wameeleza kuwa na hapa ninawanukuu: ” Bahari hii ni ya nchi tano zenye ukanda wa pwani; na kwa utaratibu nchi hizo ndizo zinapasa kuchukua uamuzi ili kuhakikisha usalama unakuwepo katika Bahari ya Kaspi na  zinapasa kuchukua maamuzi pia kuhsu kadhia nyingine kuhusiana na bahari hiyo,’ mwisho wa kunukuu.

Kamanda Irani ambaye aliwasili Jumapili jioni aliwasili St.Peterburg alitoa hotuba jana Jumanne alitoa hotuba mbele ya hadhira ya makamanda wenzake ambapo alisisistiza kuwa eneo la Bahari ya Kaspi halipaswi kuongozwa na madola ajinabi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *