#HABARI: Mahakama ya Wilaya ya Kyerwa Oktoba 8, 2025, mkoani Kagera, imesoma hukumu ya kesi ya jinai ya ubakaji dhidi ya Thobias Thomas.

Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani akikabiliwa na shtaka la kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 15, tukio ambalo lilitokea tarehe 10 Julai 2025 katika Kijiji cha Rwabigaga, Wilaya ya Kyerwa, Mkoa wa Kagera.

Baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote, Mahakama ilimtia hatiani mshtakiwa Thobias Thomas kwa kosa la ubakaji, kinyume na kifungu cha sheria husika cha Kanuni ya Adhabu (Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania).

Kutokana na hatia hiyo, Mahakama imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela.

Hukumu hiyo imesomwa na Mheshimiwa Allen Ifunya – Hakimu Mkazi Mwandamizi (SRM), mbele ya Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Sajenti Jumanne Gosberth.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *