Amir-Saeed Iravani, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa, amesisitiza kuwa: “Hali ya eneo la Magharibi mwa Asia ni mbaya mno, na hali hiyo ni matokeo ya uingiliaji kati na siasa za kijeshi za baadhi ya madola ya nje ya eneo, migogoro ya silaha inayoendelea, kukaliwa kwa mabavu kwa muda mrefu na mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni.”

Balozi Iravani alisema hayo Jumatatu Oktoba 6 katika Kamati ya Pili ya Umoja wa Mataifa  na kueleza kwamba, hiii leo msimamo wa upande mmoja unatishia ulimwengu na kudhoofisha misingi ya amani, utulivu na maendeleo kuliko wakati mwingine wowote. Vitisho hivi lazima vikataliwe kwa uamuzi na kwa pamoja,”

Kile ambacho dunia inahitaji kwa dharura leo si mgawanyiko, bali ni kuimarisha ushirikiano wa pande nyingi, ushirikiano wa kweli, mshikamano, na hatua za pamoja katika mhimili wa Umoja wa Mataifa.

Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa: Tarehe 13 Juni 2025, utawala wa Kizayuni kwa uungaji mkono wa Marekani ulianzisha hujuma kubwa ya kijeshi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na baadaye tarehe 22 Juni Tel Aviv na Washington zikafanya mashambulizi haramu dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran vinavyofanya shughuli zake kwa malengo ya amani. Uchokozi huu ulikuwa ukiukaji wa wazi wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa, sheria za kimataifa na sheria za kimataifa za kibinadamu.

Iravani alibainisha: Katika mashambulizi haya, raia, hospitali, taasisi za vyombo vya habari, na miundombinu muhimu ililengwa kwa makusudi, jambo ambalo lilidhoofisha amani na usalama wa kimataifa na kuhatarisha pakubwa Mkataba wa Kuzuia Uzalishaji na Uenezaji wa Silaha za Nyuklia (NPT)

Kwa kuzingatia hali ya leo ya kimataifa na eneo la Asia Magharibi, kudumisha uhuru wa kisiasa wa nchi kumekuwa muhimu zaidi kuliko hapo awali. Mojawapo ya changamoto za kimsingi kwa maendeleo endelevu na utulivu wa kikanda ni hali ya uchukuaji maamuzi kwa upande mmoja na uingiliaji kati wa kigeni, ambayo, kwa kupuuza kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa, husababisha kukosekana kwa utulivu, kuzusha mvutano, na kudhoofisha mamlaka ya kitaifa wa nchi.

Uchukuaji maamuzi kwa upande mmoja hutimia pale nchi au nguvu kubwa duniani inapofanya na kuchukuaa maamuzi bila kuzingatia maslahi na maoni ya nchi nyingine. Mbinu hii mara nyingi huambatana na vikwazo vya kiuchumi, mashinikizo ya kisiasa, uingiliaji kati wa kijeshi na uungaji mkono kwa makundi ya kigaidi.

Uingiliaji kati wa nchi za kigeni pia unajumuisha uingiliaji wa moja kwa moja au usio wa moja kwa moja katika masuala ya ndani ya nchi kwa lengo la kubadilisha muundo wao wa kisiasa, kiuchumi, au kitamaduni.

Matokeo mabaya ya msimamo wa upande mmoja katika kanda ni kudhoofika kwa mamlaka ya kitaifa, kuongezeka kwa mivutano ya kikanda, ukosefu wa usalama, na kuvuruga mwenendo wa maendeleo ya kiuchumi. Marekani na serikali za Magharibi, hususan katika miaka ya hivi karibuni, zimezidisha uingiliaji kati wao katika eneo la Asia Magharibi, na hilo kuwa na athari hasi za kiusalama, kiuchumi na kisiasa katika eneo.

Si hayo tu bali uingiliaji kati wa kigeni unadhoofisha uhuru wa nchi na kusababisha utegemezi wa kisiasa na kiuchumi. Kutwisha sera za upande mmoja pia kunasababisha kujitokeza ubaguzi hatari na mashindano ya uharibifu katika kanda. Vikwazo na mashinikizo ya kiuchumi ya upande mmoja pia huzuia ukuaji wa uwekezaji, biashara, na ushirikiano wa kikanda.

Hata hivyo, nchi huru na zisizokubali kuburuzwa zinaweza kupinga hatua za uingiliaji kati kwa kuwa na maamuzi mamoja na ushirikiano katika maeneo mbalimbali ya kisiasa, kiuchumi na kiusalama. Ushirikiano kati ya nchi za kanda katika mfumo wa mashirika ya kikanda kama vile Shirika la Ushirikiano la Shanghai, Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi, ECO na katika ngazi ya kimataifa katika kundi la BRICS na hivyo kuzuia satwa na kupenda kujitanua wa mataifa ajinabi.

Moja ya mikutano ya  Shirika la Ushirikiano la Shanghai,

Anuwai ya mahusiano ya kiuchumi, kuimarisha miundombinu ya ndani, na kupunguza utegemezi kwa mataifa ya kigeni ni mambo madhubuti ambayo yataimarisha ushirikiano wa kikanda ili kukabiliana na hatua za uingiliaji kati wa kikanda.

Kukabiliana misimamo na uchukuaji maamuzi ya mmoja na kuzuia uingiliaji wa  sio tu ni hitajio la kisiasa na kiusalama, bali pia ni hatua ya msingi kuelekea kupatikana amani ya kudumu, ustawi wa pande zote na kuhifadhi heshima ya mataifa. Kwa kutegemea ushirikiano wa kimataifa, diplomasia tendaji na amilifu, na kuimarisha uwezo wa ndani ni mambo ambayo bila shaaka ayanaweza kukabiliana vyema na mashinikizo kutoka nje na kuweka njia ya uhuru na maendeleo.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuzingatia misingi ya siasa zake za nje na kuheshimu uhuru na maamlaka ya mataifa mengine na kusisitiza ulazima wa kusitishwa uingiliaji kati wa Marekani na nchi za Magharibi, daima imekuwa na nafasi yenye taathira katika kuweka uthabiti na usalama katika eneo hili, na nchi huru daima zimekuwa zikiukaribisha mtazamo huu wa Iran.

Ushirikiano na mitazamo ya pamoja ya kieneo baina ya nchi huru kutapelekea utulivu wa kudumu, usalama na ustawi wa kiuchumi. Hii ni katika hali ambayo, kwa tajiriba ya kihistoria, hatua za Marekani na nchi za Magharibi katika eneo hili hazijawa na natija yoyote ghairi ya ukosefu wa uthabiti na kuvuruga usalama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *