Kaburi la Waziri wa Sheria wa zamani Robert Badinter, ambaye linatazamiwa kuingia kwenye makavazi ya kitaifa ya Pantheon, leo Alhamisi, Oktoba 9, limeharibiwa katika makaburi ya Paris ya Bagneux, manispaa ya mji wa eneo hili la Hauts-de-Seine imeliambia shirika la habari la AFP.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Manispaa ya jiji imetaja uwepo wa “vitambulisho kwenye kaburi ambavyo vinakashifu ahadi zake dhidi ya hukumu ya kifo na kuharamisha ushoga.” “Aibu kwa wale ambao wametaka kuchafua kumbukumbu yake,” ameshutumu Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Robert Badinter alifariki mnamo mwezi Februari 2024. Uharibifu wa kaburi la mwanaharakati aliyepambana dhidi ya kufutwa kwa adhabu ya kifo nchini Ufaransa unafanyika kabla kuingia kwenye makavazi ya kitaifa ya Pantheon leo Alhamisi, wakati wa sherehe rasmi itakayoongozwa na Emmanuel Macron.

Rais Emmanuel Macron ameshutumu “wale ambao wametaka kuchafua kumbukumbu” ya Robert Badinter kwa kunajisi kaburi lake katika makaburi ya Bagneux, saa chache kabla ya waziri huyo wa sheria wa zamani kuingizwa kwenye makavazi ya kitaifa ya Pantheon. “Kaburi la Robert Badinter limeharibiwa. Aibu kwa wale waliotaka kuchafua kumbukumbu yake. Usiku wa leo, ataingia Pantheon, nyumba ya milele ya dhamiri na haki,” Emmanuel Macron ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X. “Jamhuri daima ina nguvu kuliko chuki,” ameongeza.

“Kitendo cha kikatili,” kulingana na meya wa Kikomunisti wa Bagneux

Meya wa Kikomunisti wa Bagneux, Marie-Hélène Amiable, amelaani “kitendo cha kikatili.” “Maandishi yaliyopatikana na polisi yanastumu ahadi zake dhidi ya hukumu ya kifo na kuharamisha hukumu dhidi ya ushoga,” meya ameshutumu. “Hawafai kwa waziri huyu wa zamani na seneta, ambaye alikuwa msukumo wa maendeleo ya kihistoria ambayo yalisababisha kukomeshwa kwa hukumu ya kifo nchini Ufaransa mnamo mwaka 1981 na kukomesha hukumu dhidi ya ushoga mnamo mwaka 1982,” ameshutumu katika taarifa.

“Unaweza kuharibu kaburi, lakini si dhamiri,” Juliette Méadel, Waziri wa Masuala ya Miji anayeondoka na mwakilishi aliyechaguliwa huko Montrouge, mji jirani wa Bagneux, ameandika katika mtandao wa kijamii wa X. “Robert Badinter ni dhamiri na taswira ya Jamhuri, na hakuna mtu atakayeondoa hilo kutoka kwetu.” 

Uchunguzi utafabywa na idara ya usalama ya eneo la Hauts-de-Seine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *