
Kwa mujibu wa shirika hilo “Juhudi hizi zinawezekana kupitia njia za amani zilizokubaliwa na huduma za jamii.”
UNICEF imebainisha kuwa chanjo za kawaida huko Darfur zinaendelea sambamba na huduma zingine muhimu za afya ili kupambana na milipuko ya magonjwa yanayoweza kuzuilika.
Juhudi zimezaa matunda
Katika taarifa yake iliyotlewa mjini Geneva Uswis UNICEF imeongeza kuwa “mafanikio haya yanatokana na mikakati ya kuunganisha utoaji wa chanjo na huduma zingine muhimu kama usafi wa mazingira, lishe, na elimu ya afya.”
Hii inahakikisha kuwa watoto wanapata kinga kamili dhidi ya magonjwa, huku familia zao zikipokea taarifa muhimu kuhusu kinga za kiafya
Shirika limesisitiza kuwa mafunzo ya jamii na uhusiano na viongozi wa kijamii ni muhimu katika kufanikisha upatikanaji wa chanjo kwa maeneo yenye changamoto za usalama.
Njia hizi za kijamii limesema zinasaidia kupunguza hofu na kuhamasisha familia kuhakikisha watoto wao wanapata chanjo kwa wakati.
Aidha, UNICEF imeongeza kuwa ushirikiano na mashirika ya kiraia na serikali ni msingi wa kuhakikisha huduma za afya zinapatikana kwa njia endelevu.