Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi katika kanda ya Afrika Magharibi na Kati Abdouraouf Gnon-Konde, amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva nchini Uswisi kwamba takriban watu milioni nne sasa wameyakimbia makazi yao kutoka kwenye nchi za Burkina Faso, Mali, Niger na nchi jirani ya hizo, na idadi yao inakaribia theluthi mbili zaidi, ikilinganishwa na idadi ya miaka mitano iliyopita.

Baadhi ya sababu ya watu kukimbia makazi yao

Gnon-Konde amesema hali hii inaashiria ukosefu wa usalama, upatikanaji mdogo wa huduma na njia za kukidhi maisha, pamoja na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *