Akiwa Beirut, al-Shaibani amesema ziara yake imedhihirisha mtazamo mpya wa Syria kuelekea Lebanon, unaohusisha heshima kwa mamlaka ya nchi hiyo na kutoingilia masuala yake ya ndani.

Katika mkutano wa pamoja na mwenzake wa Lebanon Youssef Raggi, al-Shaibani amesema pamoja na Lebanon, wanataka kutatua vikwazo vya zamani.

Kwa upande wake,  Raggi amesema kuwa taifa hilo jirani linachukuwa mwelekeo mpya.

Masuala yanayoangaziwa katika ziara ya al-Shaibani Lebanon

Masuala muhimu yanayozungumziwa ni pamoja na hatima ya wafungwa wa Syria katika jela za Lebanon na kuwekewa mipaka kwa barabara ya mpakani ya umbali wa  kilomita 330 inayotumika kwa shughuli za magendo.

Baada ya mkutano na Rais Joseph Aoun, Shaibani amesema suala la wakimbizi litatatuliwa hatua kwa hatua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *