Mgombea Urais wa Zanzibar, Ameir Hassan Ameir wa chama cha MAKINI ameahidi kuimarisha miundombinu ya bandari ya majahazi iliyopo Malindi ili kuongeza ufanisi wa shughuli za uzalishaji mali zinazofanywa na wachukuzi na wafanyakazi wa majahazi.

Ameir amewapa ahadi hiyo wapiga kura hao alipowatembelea kwenye maeneo yao ya kazi ikiwa ni sehemu ya kampeni zake kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

#AzamTVUpdates
Mhariri | @moseskwindi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *