Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mwanza limewaelekeza waumini wake kuanza mfungo maalum wa kuombea amani ya Tanzania kuanzia Alhamisi, Oktoba 23, 2025, hadi matokeo ya Uchaguzi Mkuu yatakapotangazwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Hassan Kabeke, amesema hatua hiyo inalenga kuiombea nchi amani na mshikamano, akisisitiza kila Mtanzania ana wajibu wa kulinda amani hiyo.
✍Mwandishi Wetu
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates