#HABARI: Mahakama Kuu Masijala Ndogo Dar es salaam leo Oktoba 13,2025, imetoa uamuzi mdogo wa pingamizi lililoibuliwa na upande wa Jamhuri, juu ya maelezo ya shahidi yaliyoombwa na mshitakiwa kupokelewa na mahakama, ili ayatumie katika maswali ya dodoso ambapo pingamizi la jamhuri limetupiliwa mbali.
Mshitakiwa katika shauri hilo ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu anayekabiliwa na kesi ya uhaini ambayo sasa ipo katika hatua ya usikilizwaji.
Hata hivyo tayari Mahakama imepokea maelezo hayo na Lissu anaendelea kumuhoji shahidi.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.