#HABARI: Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeahidi kitaendelea kusimamia ubora wa elimu katika Jimbo la Peramiho na kuongeza miundombinu ya vyumba vya madarasa 255 ili kuwezesha wanafunzi kupata elimu katika mazingira bora zaidi.

Hayo yamebainishwa na Mgombea Ubunge Jimbo la Peramiho, Bi. Jenista Mhagama, akiwa katika Kijiji cha Lipokela, Kata ya Mbingamharule akinadi Sera za CCM kupitia ilani ya uchaguzi ya chama hicho na kuomba ridhaa kwa wananchi kukipigia kura ya ndio chama hicho ili kiendelee kuwaletea maendeleo.

Amesema kupitia ilani ya CCM, zaidi ya vyoo vya 150 vitajengwa katika shule zote za msingi katika Jimbo la Peramiho.

Kuhusu elimu ya Sekondari, Bi. Mhagama amesema kuwa Serikali ya CCM inayomaliza muda wake imefanya kazi kubwa ya kuboresha ubora wa elimu na sasa ufaulu wa wanafunzi wa Sekondari umeongezeka kutoka asilimia 76 hadi 97 ndani ya kipindi cha miaka mitano.

Bi. Mhagama amewaomba wananchi ifikapo Oktoba 29, 2025 kushiriki kwenye uchaguzi mkuu na kukipigia kura ya ndio CCM kupitia wagombea wake kuanzia Mgombea Urais Dkt Samia Suluhu Hassan, yeye mwenyewe anayegombea nafasi ya Ubunge pamoja na Madiwani wagombea kupitia CCM.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *