Mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameahidi kuendelea kujenga viwanja 17 vya kisasa vya michezo ili kuwasaidia wanamichezo kuwa na maeneo ya kufanyia mazoezi na mashindano ya kitaifa na kimataifa.
Mgombea huyo ametoa ahadi hizo ikiwa ni mwendelezo wa kampeni zake za makundi kwa lengo la kuomba kura, ambapo amekutana na kufanya matembezi ya mazoezi na wanamichezo. MatembezI hayo yalianzia Viwanja vya Bwawani hadi Viwanja vya Maisara, Mjini Unguja amesema Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupitia ilani yake inayomaliza muda, imetekeleza kwa vitendo ujenzi na ukarabati wa viwanja mbalimbali, hivyo dhamira yake ni kuifanya sekta ya michezo kuwa bora zaidi.
✍Mtumwa Said
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates