#HABARI: Zoezi la uthamini maeneo yatakayopitiwa na ujenzi wa Mradi wa Reli ya Kisasa SGR kipande cha 6 kutoka Tabora hadi Kigoma linaendelea kwa kasi katika wilaya sita za mikoa hiyo.

Wilaya hizo ni Tabora Mjini, Uyui, Urambo, Kaliua, Uvinza pamoja na Wilaya ya Kigoma.

Timu kutoka Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali ikiongozwa na Mthamini Kiongozi FRV James Mark Mwanakatwe ipo mkoani Kigoma ikiendelea na kazi ya uhamasishaji pamoja na ukusanyaji taarifa za mali uwandani kwa wananchi ambao maeneo yao yanaguswa na mradi huo.

Kwa mujibu wa FRV Mwanakatwe, timu yake imeshafanya uthamini wa vipande 52 (Land Parcel) ikiwemo kipande cha daraja la mto Malagarasi lenye urefu Km 3 ambalo liko katika hatua za mwisho za utekelezaji.

Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *