#HAARI: Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Dalmia Mikaya, amepongezwa kwa hatua kubwa za kuboresha Mazingira ya Utendaji wa Baraza la Wazee la Ushauri la Wilaya ya Kigamboni, ikiwemo kuwapatia ofisi mpya ya kisasa.
Pongezi hizo zimetolewa leo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Dar es Salaam, Mzee Ramadhani Matimbwa.
Mzee Matimbwa amesema ofisi waliyopewa imeongeza ari na hadhi ya Baraza hilo, na kutoa wito kwa wilaya nyingine jijini Dar es Salaam kuiga mfano huo.
Uboreshaji huo unatajwa kuongeza ufanisi wa Baraza la Wazee katika kutoa ushauri na kushiriki kwenye masuala ya kijamii na maendeleo katika Wilaya ya Kigamboni.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.