HALMASHAURI SONGWE YAPATA VIONGOZI WAPYA
#HABARI: Wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe, iliyopo mkoani Songwe, wamemchagua kwa kura za ndio Bw. Abraham Sambila, ambaye ni Diwani wa Kata ya Mbagala, kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, pamoja na Bw. Godian Wangala, ambaye ni Diwani wa Kata ya Totowe, kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, ambao wote wamepata jumla ya kura 25 za ndio. Uchaguzi huo ulisimamiwa na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Bw. Godfrey Kawacha.
Bw. Sambila, baada ya kuapishwa ameahidi kujikita kuliongoza vyema Baraza hilo huku akiwaomba Madiwani kuhakikisha wanatumia vizuri nafasi zao katika kuwaletea maendeleo wananchi katika kata zao.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania