#HABARI: Jeshi la Polisi Tanzania limetoa taarifa kuhusu mambo mbalimbali yanayoendelea kwenye mitandao ya kijamii hususan ‘maandamano’ yanayotajwa kufanyika Desemba 9, 2025.

Jeshi hilo limesema, linaendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kulinda maisha ya watu na mali zao sambamba na kuhakikisha hali ya amani, utulivu na usalama unaendelea kuimarika nchini.

Pia, limeendelea kuzuia uhalifu sambamba na kuwakamata wale wanaofanya makosa mbalimbali yakiwemo makosa ya kimtandao kama yale ya wanaoendesha makundi mbalimbali katika mitandao ya kijamii ya kuhamasisha uhalifu na kuwachulia hatua kama sheria za nchi zinavyoelekeza.

Aidha, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama vimekuwa vikifuatilia kwa karibu sana yanayoendelea katika mitandao ya kijamii na kwenye makundi sogozi wakihamasisha wanayo yaita
maandamano ya amani yasiyo na kikomo Disemba 09, 2025.

Hicho wanachohamasisha na kukiita maandamano ya amani mtu yeyote aliyewasikiliza na akaendelea kuwasikiliza wanahamasishana kufanya mambo yafuatayo;

1. Siku hiyo ya maandamano yasiyo na kikomo yaani Disemba 9, 2025 wanaelekezana ambaye hajui kutumia silaha na hajapitia mafunzo siku hiyo asishike silaha wawaachie waliopata mafunzo ya matumizi ya silaha.(Kwa maana rahisi watu hawa wanazo silaha za kutimiza lengo ambalo wamekusudia).

2. Kupitia mitandao na klabu mbalimbali za mtandaoni wanahamasishana ili kusiwe na shughuli yoyote itakayokuwa inaendelea.

3. Pia wahakikishe wanaharibu na kuchoma moto minara yote ya mawasiliano ili nchi nzima ikose mawasiliano.

Swipe kusoma zaidi. Unaweza pia kuitazama video kamili Youtube>>> https://www.youtube.com/watch?v=qGAl1ZHvpJM

Powered by #MCHEZOSUPA:

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *