Huduma za mabasi yaendayo haraka katika Barabara ya Morogoro… kutoka Kimara kuelekea Gerezani – Kivukoni na Morocco – zimerejea rasmi leo kufuatia agizo la Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba aliyetaka huduma hiyo irejee mara moja.
Farasi imezungumza na baadhi ya abiria ambao wameeleza kufurahishwa na kurejea kwa usafiri huo, wakisema kumerahisisha safari zao na kupunguza usumbufu waliokumbana nao wakati huduma iliposimama.
#AzamTVUpdates
Juliana James
Mhariri | John Mbalamwezi