#HABARI: Wakati msimu wa kilimo ukiwadia, Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe, mkoani Songwe, imetangaza neema kwa wakulima na wafugaji kwa kuanza mikakati ya kuimarisha sekta za Kilimo na Mifugo, ikiwa ni pamoja na kuongeza uzalishaji wa mazao ya ufuta, Tumbaku na mazao ya chakula kwa kusambaza na kugawa mbegu bora pamoja na mbolea.

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali katika kipindi ambacho baraza hilo lilivunjwa kupisha Uchaguzi Mkuu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmasauri hiyo CPA. Cecilia Kavishe, amesema katika msimu huu wa kilimo wanatarajia kununua na kusambaza mbegu za ufuta tani tano, mbegu za mbaazi tani tatu, mbegu za mahindi tani kumi na nane nukta moja huku zaidi ya tani elfu nne za mbolea zikiwa zimesambazwa mpaka sasa.

CPA. Cecilia ameongeza kuwa Halmashauri hiyo imeendelea kutoa chanjo za mifugo dhidi ya ugonjwa wa homa ya mapafu kwa Ng’ombe pamoja na chanjo ya ugonjwa wa kideri kwa kuku, huku akielezea kuwa hali ya upatikanaji wa chakula imeendelea kuimarika.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *