Kampuni ya bima ya CRDB (CIC) imetumia zaidi ya shilingi bilioni tano kama fidia kwa wateja takribani 1,000 mwaka huu, imeelezwa.
Akizungumza na menejimenti ya CIC, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, amesema fidia hizo zinaonyesha uimara wa huduma za bima na umuhimu wake katika kuzuia wananchi kuangukia kwenye umasikini pale majanga yanapotokea.
Ameongeza kuwa, mwenendo huo utaongeza imani ya Watanzania kutumia bima kama chombo cha kujilinda kiuchumi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa CIC ambayo ni kampuni tanzu ya Benki ya CRDB, Wilson Mnzava, ameeleza kuwa hadi mwishoni mwa Oktoba 2025, kampuni hiyo imesajili wateja zaidi ya 40,000 huku wateja 833 wakipatwa na majanga yaliyosababisha uharibifu wa mali zao.
Amesema fidia hizo, zilizofikia shilingi bilioni 5.3, zimewawezesha wateja kuendelea na shughuli zao bila kukwama huku CIC ikipata faida ya zaidi ya shilingi bilioni 2.7 baada ya kodi.
✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates