Wafanyabiashara nchini wanatarajiwa kupata ahueni ya mitaji ya biashara kupitia mpango wa mkopo wa kupata mali za biashara ‘Asset Finance’ baada ya Benki ya I&M Tanzania kuingia kwenye ushirikiano na kampuni ya Hanspaul wa kuimarisha upatikanaji wa huduma hiyo kwa wateja wake nchini.
Kupitia mpango huo, benki itatoa ufadhili wa hadi asilimia 90 ya thamani ya mali, huku marejesho yakiwa ya hadi miezi 60, pamoja na huduma zinazokamilisha mchakato mzima wa umiliki wa mali.
Hatua hiyo inalenga kusaidia kampuni zinazohitaji magari ya safari, mabasi ya watalii na vifaa maalumu vinavyotumika kwenye shughuli za biashara kama utalii, hasa katika mikoa kama Arusha ambao ni kitovu cha vivutio vya utalii.
I&M Bank inasema uwekezaji huo unalenga kupunguza mzigo wa mitaji mikubwa kwa biashara ndogo na za kati, ambazo ndizo msingi wa shughuli nyingi za kiuchumi Tanzania.
Mkuu wa Matawi na Wateja Wadogo na wa Kati wa I&M Bank Tanzania, Yusuf Mdoe, amesema ushirikiano na Hanspaul utawapa uwezo wa kutekeleza mpango huo kwa ufanisi.
Mpango huo unatarajiwa kuongeza ufanisi, ubunifu na ushindani katika sekta ya utalii, huku ukitoa mwanya wa ukuaji kwa maelfu ya biashara zinazotegemea mali za kibiashara kuendesha shughuli zao.
✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates