#HABARI: Moto mkubwa umeteketeza sehemu ya Hifadhi ya Mlima Hanang, uliopo wilayani Hanang mkoani Manyara na kusababisha uharibifu wa misitu na viumbe hai vilivyopo kwenye hifadhi hiyo ambapo chanzo cha moto huo bado hakijajulikana huku juhudi za Jeshi la Zimamoto Wilaya ya Hanang zikiendelea kwa kushirikiana na wananchi kuzima moto huo.

Akizungumza kwa njia ya simu Mhifadhi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Hifadhi ya Mlima Hanang, Abubakari Mpapa amesema moto huo umekua na athari katika shughuli za uhifadhi na kuongeza kuwa juhudi kubwa zinafanywa na jeshi la zimamoto ambao watatoa taarifa rasmi za moto huo.

ITV imemtafuta Kamanda wa Zimamoto Wilaya ya Hanang kwa njia ya simu ambapo simu yake imeita bila kupokelewa.

ITV inaendelea kufuatilia tukio hili kwa ukaribu na itakuletea kila kitakacho jiri.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *