#HABARI: Watu wawili wa Kitongoji cha Itwili, Kijiji cha Old Shinyanga, ambao ni Mama na mtoto wake wa kike, Suzana Samweli (41) na Happyness Peter (20), wamefariki dunia baada ya kufukiwa na kifusi cha mchanga wakati wakichimba Madini ya ujenzi aina ya Kokoto katika eneo lisilo rasmi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga, ikisubiri kukabidhiwa familia kwa ajili ya maziko.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji, Bw. Doto Bwire, ameeleza kuwa eneo la ajali ni hatarishi na kuwataka wananchi kutochimba mchanga au kokoto kwenye maeneo yasiyoruhusiwa kisheria.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *